nyumba ya sala kwa mataifa yote
The Power of Perfection International Ministries ni familia inayoongozwa na Roho ikiinua kizazi kinachomwabudu Mungu katika roho na kweli.
The Power of Perfection International Ministries ni taasisi ya Kiroho iliyoanzishwa mwaka 2016 chini ya mbeba maono, Mtume na Nabii wa Bwana, Senior Prophet Jackson Ibrahim.
Huduma hii ina lengo la kung’oa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza misingi mibovu ya miungu ambayo imekuwa ikizitesa koo na familia nyingi hapa duniani, kisha kumuinulia Mungu kizazi kitakachomtumikia na kumtegemea yeye katika mambo yote ya roho na mwili.
Makao yetu makuu yako Kwa Morombo jijini Arusha, na matawi yake Mirerani mkoani Manyara na Mbezi Beach Makonde jijini Dar es Salaam. Maono yetu ni kufikia kila mtaa, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na mataifa yote, tukimuinulia Mungu kizazi kitakachomwabudu katika roho na kweli.
Kung’oa & kubomoa
Kubomoa misingi mibovu ya kiroho iliyo kinyume na ufalme wa Mungu katika familia kote duniani.
Kujenga & kuinua
Kuinua kizazi kinachoishi kwa kumtegemea Mungu katika roho, nafsi na mwili, kwa kuwa Kristo ni yote katika yote.
Kufikia mataifa
Kupeleka injili kila mtaa, kijiji, wilaya na taifa hadi Mungu aabudiwe kila mahali.

Senior Prophet Jackson Ibrahim
Senior Prophet Jackson Ibrahim ni mbeba maono wa The Power of Perfection International Ministries: kung’oa, kubomoa na kujenga upya misingi mibovu ya kiroho, na kumuinulia Mungu kizazi kinachomtumikia na kumtegemea katika roho, nafsi na mwili.